Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania, Maharage Chande
akizungumza kuhusu msaada ambao wameutoa kwa kituo cha Al--Madina.
Zikiwa zimesalia siku kadhaa kabla ya kusherekea sikukuu ya Eid El
Fitri, Kampuni ya Multichoice Tanzania ambao ndiyo wasambazaji wa
ving'amuzi vya DSTV nchini imetoa msaada wa vitu mbalimbali kwa watoto
yatima ambao wanaishi katika kituo cha Al-Madina kilichopo Tandale kwa
Tumbo, misaada ambayo kwa namna moja au nyingine inaweza kusaidia
kubadilisha maisha ya watoto hao.
Misaada ambayo imetolewa kwa
watoto hao ni Cherehani 4, kapeti 12, vikombe 60, sahani 40, magodoro
11, shuka 40, tenga za nguo 3, jagi 6, beseni kubwa 3, sufuria 9, chupa
za chai 4 na mikeka 6.
Akizungumzia misaada hiyo, Mkurugenzi
Mtendaji wa Multichoice Tanzania, Maharage Chande alisema msaada huo ni
mwendelezo wa misaada ambayo Multichoice imekuwa ikitoa kwa kituo hicho
kwa lengo la kuwasaidia kuishi maisha bora lakini pia kuwapatia msaada
ambao unaweza kuwasaidia kuwa na uwezo wa kuingiza kipato.
"Multichoice tumekuwa tukitoa misaada yetu kwa kituo hiki tangu 2009 na
leo tumewaletea mwingine ikiwa ni kila mwaka tunafanya hivyi lakini kwa
mwaka huu tumeleta pia Cherehani ambazo zitawasaidia kupata kipato,
"Pamoja na hayo pia tumewafungia king'amuzi ambacho watoto watakuwa
wakiangalia vipindi balimbali baada ya kurejea nyumbani na tuna chaneli
mbalimbali za vipindi vya watoto na burudani kwahiyo tunaamini kuwa
watoto watafurahi," alisema Chande.
Nae mlezi wa kituo hicho, Bi.
Kuruthum Yusuf aliwataja Multichoice kama kampuni ambayo imekuwa mstari
wa mbele kuwapatia misaada na kuyaomba makampuni mengine kuwa na
utaratibu kama wa Multichoice wa kuwasaidia misaada kutokana na kuwa na
idadi kubwa ya watoto ambao wanahitaji misaada ili kuboresha maisha yao.
Mlezi wa kituo cha watoto yatima cha Al-Madina akizungumza kuhusu
msaada ambao wamepokea na jinsi ambavyo Multichoice Tanzania imekuwa
ikiwapatia misaada. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice
Tanzania, Mharage Chande.
"Tangu walipotufahamu wamekuwa
wakitupatia misaada kila mwaka, niwashukuru sana kwa moyo wao na kutoa
sio utajiri ila tu wana moyo wa kutoa na hata wenngine wanatakiwa kuwa
na moyo kama wao (Multichoice) wa kusaidia," alisema Bi. Kuruthum.
Pamoja na hayo pia, Bi. Kuruthum alieleza kuwa kwa sasa bado
wanakabiliwa na changamoto ya vifaa vya shuleni kwa watoto ambao
wanasoma.
Kutokana na msaada ambao umetolewa na Multichoice kwa
watoto wa kituo cha Al-Madina ambacho kina watoto 57, wasichana wakiwa
ni 23 na wavulana ni 34 basi ni wazi kuwa kama wakitumia msaada huo
vyema basi kwa namna moja au nyingine wanaweza kubadilisha maisha yao
kwa hatua fulani ambayo awali hawakuwa nayo kama vile kutumia cherehani
kwa kushona nguo na kujiongezea kipato.
Meneja Uhusiano na Masoko wa Multichoice Tanzania, Furaha Sumalu akitoa
neno la ufunguzi kuhusu misaada ambayo imekuwa ikitolewa na Multichoice
Tanzania pamoja na historia fupi ya kituo hicho.
Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania, Mharage Chande akimkabidhi
Cherehani, mlezi wa kituo cha Al-Madina, Kuruthum Yusuf. Wa tatu
kushoto ni Meneja Uhusiano na Masoko wa Multichoice Tanzania, Furaha
Samalu wakiwa na wafanyakazi wengine wa Multichoice Tanzania.
Meneja Uhusiano na Masoko wa Multichoice Tanzania, Furaha Samalu
akimpongeza mlezi wa kituo cha Al-Madina, Kuruthum Yusuf baada ya
kukabidhiwa misaada na Multichoice Tanzania.
Wafanyakazi wa Multichoice Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja na watoto yatima wanaoishi katika kituo cha Al-Madina.
Meneja Uhusiano na Masoko wa Multichoice Tanzania, Furaha Samalu
akiwaelekeza jambo watoto wanaoishi katika kituo cha Al-Madina.
Watoto yatima wanaoishi katika kituo cha Al-Madina wakiwa katika picha ya pamoja.
Mwonekano wa vitu vilivyotolewa na Multichoice Tanzania kwa kituo cha kulelea watoto yatima cha Al-Madina.