Thursday, February 27, 2014



ronaldo_8e1ea.jpg


REAL Madrid imejihakikishia kucheza robo fainali ya michuano ya 
Ligi ya Mabingwa barani Ulaya baada ya kuitandika Schalke 04 ya Ujerumani
 mabao 6-1. Mchezaji bora wa dunia, Cristiano Ronaldo, mchezaji 
aliyevunja rekodi ya usajili ulimwenguni Gareth Bale pamoja 
na mchezaji mahiri Karim 
Benzema walihakikisha kila mmoja wao anatupia nyavuni magoli mawili ili
 kuifanya Real Madrid, vinara wa ligi kuu nchini Hispania, kuisulubu vilivyo 
Schalke 04 tena kwenda
 dimba lake la nyumbani, Veltins-Arena. Bao la kufutia machozi 
la Wajerumani hao lilifungwa
 na Klaas Jan Huntelaar katika dakika ya 90.
Alikuwa Karim Benzema katika dakika ya 13 tu alipopokea mpira kutoka kwa 
Cristiano Ronaldo na kuutumbukiza wavuni kama ishara ya ufunguzi rasmi wa 
karamu ya magoli ya miamba hao wa soka nchini Hispania. Kisha, panapo 
 dakika ya 21, mchezaji aghali zaidi aliyesajiliwa kutoka Tottenham Hotspur ya
 Uingereza, Gareth Bale akautia mpira kimiani baada ya kupokea pasi kutoka kwa 
Karim Benzema.

Mwamuzi Howard Webb, anayetajwa kuwa mwamuzi bora zaidi duniani kwa sasa 
 alipopuliza kipenga kuashiria mapumziko, Real Madrid wakarejea vyumba vya 
mapumziko wakiwa tayari na magoli mawili nunge.

Timu hizo ziliporejea dimbani kwa ngwe ya mwisho, ilimchukua Cristiano Ronaldo 
dakika saba tu kuibadili pasi kutoka kwa Gareth Bale kuwa goli la tatu. Dakika tano 
baadaye, dakika ya 57, Karim Benzem akafungua awali ya pili ya ufungaji kwa wasukuma
 ndinga hao machachari alipofunga bao la nne dhidi ya Schalke 04. Kama ilivyo
 kanuni ya hesabu za pythagoras, Karim alifunga goli hilo kwa kupata usaidizi 
kutoka kwa yule yule aliyempa pasi awali, Cristiano Ronaldo.



Dakika ya 69 ya mchezo, ikawa zamu tena ya Gareth Bale kuutia mpira wavuni baada ya 
kupokea pasi nzuri ya Sergio Ramos. Ubao wa matokeo ukasoma
 Schalke 04 0 Real Madrid 5. Matokeo hayo yalidumu kwa dakika 20 tu
 kwani panapo dakika ya 89 ya mchezo krosi ya Karim Benzema ikamfikia
 Cristiano Ronaldo. Naye hakufanya ajizi, akaitia wavuni na kuwafanya mashabiki wa
 Real Madrid kote ulimwenungi kushangilia kwa tambo na kujidai kwa kila namna.

Dakika iliyofuata, Klaas Jan Huntelaar aliyekuwa tayari amelimwa kadi ya njano
 panapo dakika ya 72, akafunga bao la kuwafutia machozi wenyeji wa mchezo huo.

Kwa matokeo hayo, Schalke 04 inahitaji miujiza ili isonge mbele. Timu hizo 
 zinatarajia kukwaana tena katika mchezo wa pili utakaokimbizwa dimbani 
 Santiago Bernabeu jijini Madrid, Hispania majuma matatu yajayo.

Kwingine barani Ulaya, Galatasaray iliikaribisha Chelsea, vinara wa 
ligi kuu ya Uingereza. Dakika ya 9 tu ya mchezo huo uliopigwa katika
 dimba la Turk Telekom, Fernando Torres akaifungia Chelsea goli la kuongoza.
 Chelsea ikawa timu ya kwanza kutoka Uingereza kufunga goli katika hatua hiyo
 ya 16 ya michuano ya UEFA. Timu zingine kutoka Uingereza, Machester City,
 Arsenal na Manchester United ziliambulia kichapo cha magoli 2-0 kutoka 
 kwa Barcelona, Bayern Munich na Olympiakos.

Chelsea iliendelea kuongoza ikiwa ugenini hadi dakika ya 65 pale Aurelien
 Chedjou alipofunga akisaidiwa na Wesley Sneijer. Matokeo hayo yanaipa ahueni ya
 goli la ugenini Chelsea. Timu hizo zinatarajia kutimuliana vumbi tena wiki tatu zijazo 
pale mitaa ya Fulham, London katika dimba la Stamford Bridge.

Tuesday, February 25, 2014


Kipindi cha pili dakika 55 Mchezaji wa Olympiakos Joel Campbell akaiongezea bao la pili  timu yake kwa kufanya 2-0 dhidi ya United baada ya mabeki wa United kufanya makosa ya ukabaji na hatimaye Joel Campbell kufunga bao hilo kwa kupewa pasi safi na Michael Olaitan.Elated: The win meant so much to the Olympiacos players, seen here celebrating the secondJoel Campbell akipongezwa baada ya kufunga bao la pili na kufanya 2-0 katika kipindi cha pili dakika 55 dhidi ya United ya England.Outstretched: De Gea is well beaten by Campbell's shot in the 53rd minute to deflate United

mkali

Down and out? Moyes slumps back into his seat after Olympiacos score their second goalMAn Utd defensive woe vs OlympiakosHDa!! Devid Moyes akiangalia kuelemewa na Olympiakos huku ikionekana wachezaji wake kucheza chini ya kiwango!!!Taswirazzzz!!!!! K!
Baada ya kufungwa bao la pili United, Dakika ya 60 kipindi cha pili wamefanya mabadiliko Shinji Kagawa akaingia kuchukua nafasi ya Tom Cleverley na huku Danny Welbeck akichukua nafasi ya Antonio Valencia.!Flat out: Robin van Persie lies on the floor after missing United's best chance of the game late onVan Persie chini baada ya kukosa bao la wazi...akiishilia kupaisha juu kwa juu!!


Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetangaza kikosi cha wachezaji 22 kwa ajili ya mechi ya kirafiki ya kalenda ya FIFA dhidi ya Namibia (Brave Warriors) itakayochezwa Machi 5 mwaka huu jijini Windhoek, Namibia.

Wachezaji walioitwa katika timu hiyo ni makipa Deogratius Munishi (Yanga), Ivo Mapunda (Simba) na Mwadini Ally (Azam). Mabeki wa pembeni ni Edward Charles (JKT Ruvu), Erasto Nyoni (Azam), Hassan Mwasapili (Mbeya City) na Michael Aidan (Ruvu Shooting).

Mabeki wa kati ni Aggrey Morris (Azam) na Kelvin Yondani (Yanga) wakati viungo ni Amri Kiemba (Simba), Athuman Idd (Yanga), David Luhende (Yanga), Frank Domayo (Yanga), Jonas Mkude (Simba) na Mwinyi Kazimoto (Markhiya Sports Club, Qatar).

Washambuliaji ni Athanas Mdamu (Alliance Mwanza), Haruna Chanongo (Simba), Khamis Mcha (Azam), Mbwana Samata (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC), Mrisho Ngasa (Yanga), Ramadhan Singano (Simba) na Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC).

Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itaingia kambini Machi 1 mwaka huu, kwenye hoteli ya Accommondia inatarajiwa kuondoka Machi 3 mwaka huu kwenda Windhoek.


Wachezaji ambao timu zao zinacheza mechi za mashindano ya kimataifa na ligi wikiendi hii wataripoti kambini mara baada ya mechi zao kumalizika.



Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) zimewaagiza wanachama wake- vyama vya mpira wa miguu vya mikoa kuwapatia orodha ya klabu zote za mpira wa miguu zilizosajiliwa katika mikoa yao.

Orodha hiyo inatakiwa kujumuisha namba ya usajili wa klabu, viongozi waliopo madarakani kwa sasa pamoja na mawasiliano yao (namba za simu na anuani za email) na eneo yalipo makao ya klabu husika.

Kwa utaratibu huo, vyama vya mikoa vitakusanya taarifa za klabu zinazocheza ligi ya mikoa, lakini wakati huo vinatakiwa kuwasiliana na wanachama wake (vyama vya wilaya) kupata taarifa za klabu zinazocheza ligi za wilaya na baadaye kuziwasilisha TFF.

Klabu ambazo taarifa zake zitakuwa hazijawasilishwa TFF hadi Agosti mwaka huu hazitaruhusiwa kushiriki ligi ya msimu wa 2014/2015 katika ngazi yoyote ile.

RAIS MALINZI KUZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi atakuwa na mkutano na waandishi wa habari juu ya programu ya mpira wa miguu kwa vijana.

Mkutano huo utafanyika kesho (Februari 26 mwaka huu) saa 5 asubuhi kwenye ofisi za TFF zilizopo ghorofa ya 3 katika Jengo la PPF Tower, mtaa wa Garden na Ohio.

*AZAM, ASHANTI UNITED KUKIPIGA VPL
Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara inaendelea kesho (Februari 26 mwaka huu) kwa mechi moja itakayochezwa Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi jijini Dar es Salaam.


Mechi itazikutanisha timu za Azam inayoshika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi 37 dhidi ya Ashanti United iliyoko nafasi ya 12 kwa pointi zake 14.
2w650c0.bild_Jose Mourinho ametoa ishara kwamba klabu yake ya Chelsea inaweza kutuma ofa ya kumsajili mshambuliaji wa kikolombia Radamel Falcao mara tu dirisha la usajili litakapofunguliwa.
Meneja huyo wa Chelsea hakuonyesha kuficha matamanio yake ya kumleta mshambuliaji huyo wa Colombia darajani – Falcao ambaye kwa sasa ni majeruhi wa goti – ameripotiwa kwamba anataka kuondoka kwenye ligi kuu ya Ufaransa kutokana na kutokuwepo kwa ushindani kwenye ligi hiyo.
Katika mahojiano na Canal Football Club, Mourinho aliondoa uwezekano wa klabu yake kuwasajili washambuliaji wa PSG  Zlatan Ibrahimovic na Edinson Cavani, akisisitiza ni ‘haiwezakani’ kuwasajili wachezaji hao.
Alisema: ‘Nina timu, lakini sina mshambuliaji. Falcao hana timu pale. Mchezaji kama yeye hawezi kuwa anacheza mbele ya mashabiki 3,000. Monaco ni klabu ya kumalizia soka, hampafai pale kwa sasa.”
Falcao, 28, alijiunga na Monaco kwa ada ya £50million kutoka Atletico Madrid kipindi cha kiangazi kilichopita.

                                      

TFC_1_93eff.png
TFC_2_a952e.png
Chanzo, soccerway.com, R.M

LIGI KUU TANZANIA BARA

Imetumwa kwenye Michezo

TFC_1_93eff.png


Baadhi ya safu ya wanenguaji mahiri wa kiume wa Extra Bongo.
Amini akishoo Love na Linah (kushsoto) pamoja na mwimbaji wake.
Baadhi ya safu ya wanenguaji wa kike mahiri wa Extra Bongo.
Wanenguaji katika pozi poa.
Khadija Kopa na Abdul Misambano wa TOT.
Khadija Kopa, Misambano na 'Okwi' shabiki wa Yanga.
Lina na 'back-up singer' wake.
Mamaa Winnie Masanja, mama watoto wa mwanamuziki Banza Stone.
Mke wa 'Mkubwa' Said Fela (kulia).
Mmoja wa wanamuziki wa Mashujaa Band, Gado.
TX Moshi Jnr wa Msondo Music Band.
Wadau wa Dar Live.
Wasanii Linah na Amini.


Iringa. Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Wilbrod Slaa amesema tatizo la umaskini linalowakabili Watanzania, linatokana na viongozi walioko madaraka kutokuwa waadilifu.
Alisema Tanzania ni nchi iliyojaaliwa rasilimali nyingi ambazo kama zikisimamiwa vyema taifa haliwezi kuwa na watu maskini kama ilivyo hivi sasa.
Dk Slaa alitoa kauli hiyo jana wakati akizungumza kwenye mikutano ya kampeni iliyofanyika katika Vijiji vya Igula katika Kata ya Luwota na Magulilwa mkoani Iringa.
“Nchi hii siyo maskini, imejaliwa rasilimali nyingi ambazo kama zikisimamiwa ipaswavyo, taifa lisingekuwa na umaskini kama ilivyo sasa,” alisema Dk Slaa na kuongeza:
“Leo hii viongozi wa CCM wamekosa uadilifu ndiyo maana magogo kutoka katika misitu yetu yanaibiwa na kupelekwa nje ya nchi.
Dk Slaa alisema hayo yanatokana taifa kuongozwa na watu wasio waadilifu, huku Amiri Jeshi Mkuu ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano, Jakaya Kikwete akishindwa kukabiliana na hali hiyo. Katika mikutano hiyo, Dk Slaa aliwataka wakazi wa Kalenga kumchagua mbunge wao ili kuongeza idadi ya wabunge wake


DSC_0549
Mama wa Mitindo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Fabak Fashions na wandaaji wa onyesho la Lady in Red, Bi. Asia Idarous Khamsin akizungumza na wadau tasnia ya mitindo waliojumuika kwenye After Party ya kuwashukuru wadau waliotoa michango mbalimbali tangu kuanza kwa onyesho la Lady in Red nchini Tanzania.

...Ally Rehmtulla, Martin Kadinda watunukiwa vyeti vya mafanikio
Na Andrew Chale
HALFA maalumu ya kilele cha Miaka 10 ya onesho la mavazi la ‘Lady in Red Super Brand’ usiku wa Jumamosi Februari 22, lilikuwa la aina yake kwa kuvutia watu mbali mbali ndani ya Ukumbi na mgahawa wa kisasa wa Nyumbani Lounge, ambapo pia wadau walikabidhiwa vyeti.
Tukio hilo la aina yake ambalo lilivuta umati mkubwa wakiwemo wadau wa ubunifu na mitindo nchini pamoja na watu maalufu, Pia walipata kupita kwenye zuria jekundu (red carpet) na kupata picha za ukumbusho wa tukio hilo.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Fabak Fashions na wandaaji wa onyesho hilo kila mwaka, Asia Idarous Khamsin, aliwashukuru wadau waliojitokeza kwenye halfa hiyo maalumu na kutoa vyeti kwa watu na taasisi zilizoweza kuliunga mkono onyesho hilo pamoja.
DSC_0572
Mama wa Mitindo Bi. Asia Idarous Khamsin akipozi wakati wa zoezi la kugawa vyeti na models waliovaa mavazi yaliyoonyeshwa kwenye onyesho la kutimiza miaka 10 la Lady in Red lililofanyika hivi karibuni.
“Tunamshukuru Mungu kwa kufikisha Miaka 10 ya Lady in red, hadi kufikia hapa, tumeweza kufanya mambo makubwa katika tasnia hii ya ubunifu wa mavazi na jukwaa hili litaendelea kuwa chachu ya mafanikio zaidi na zaidi” alisema Asia Idarous.
Na kuongeza kuwa, jukwaa hilo ndilo pekee lililoweza kuibua wabunifu wakubwa hapa nchini huku wengine wakipeperusha vyema bendera ya Tanzania nje ya nchi, wabunifu hao ni pamoja na Ally Rehmtullah, Martin Kadinda, Ahmed Abdul, Faustin Simon.
DSC_0577
Mwanamitindo wa siku nyingi Fiderine Iranga akipokea cheti kutoka kwa Mama wa mitindo Asia Idarous Khamsin kwa kutambua mchango wake katika tasnia ya mitindo nchini.
Wengine ambao nao wanachipukia kwa sasa akiwemo Salim Ally, Salim Ally, Abdul Mwene,Baby Julieth, Baby Masai na wengine wengi.
Asia Idarous alibainisha kuwa, wapo mbioni kuliboresha jukwaa hilo na kuwa la Kimataifa ikiwemo kushirikisha wabunifu wa kimataifa na kufungua milango kwa wabunifu wa ndani kujiuza kimataifa.
DSC_0581
Mwanamitindo mkongwe Fiderine Iranga akimkabidhi zawadi Mama wa Mitindo Bi. Asia Idarous kwenye After party ya kuwashukuru wadau waliofanikisha sherehe za kutumiza miaka 10 ya onyesho la Lady in Red iliyofanyika mwishoni mwa juma kwenye kiota cha Nyumbani Lounge jijini Dar.
Aidha, katika halfa hiyo pia wageni na wadau waliofika walipata kushuhudia shoo fupi ya mavazi yaliyobuniwa na Lucy Warere wa Tifu tifu fashions, Beda Masai na Asia Idarous Khamsini.
Asia Idarous aliwataja wadhamini waliodhamini halfa hiyo ni pamoja na Times fm, Michuzi media group, MOblog, DTV, Nyumbani Lounge, Darling air, G one Media, Channel Ten, CTN na wengine wengi.
DSC_0587
Mbunifu wa Mavazi nchini Ally Rehmtullah akipokea cheti cha shukrani ya ushiriki wa onesho la Lady in Red kutoka kwa Mama yake Mlezi Asia Idarous Khamsin.
DSC_0601
Cake ya After Party ya Onesho la Lady in Red iliyoandaliwa maalum kwa kuwashukuru wadau mbalimbali waliofanikisha sherehe za miaka 10 ya Lady in Red nchini.
DSC_0602
Honest Arroy wa 360 Degrees akikata cake kwa niaba ya wadau kwenye After Party ya Lady in Red iliyofanyika mwishoni mwa juma kwenye kiota cha Nyumbani Lounge.
DSC_0617
Model Richard akililishwa kipande cha cake na Mama wa Mitindo Asia Idarous Khamsin kama shukrani ya kushiriki maonyesho mbalimbali ya Lady in Red.
DSC_0619
DSC_0621
Wadau mbalimbali waliojitokeza kwenye After Party ya kusheherekea miaka 10 ya Lady in Red wakitazama matukio mbalimbali kwenye luninga ndani ya kiota cha Nyumbani Lounge.
DSC_0645
Mwandishi wa gazeti la Tanzania Daima, Andrew Chale akilishwa kipande cha cake na mmoja wa Models kwenye After Party ya kuwashukuru wadau waliofanikisha tangu kuanzishwa onesho la Lady in Red mpaka leo hii kutimiza miaka 10 kwenye tasnia ya mitindo nchini.
DSC_0631
Wadau wakiwa wamepozi kwenye kiota cha Nyumbani Lounge wakati wa After Party ya Lady in Red iliyofanyika mwishoni mwa juma jijini Dar.
DSC_0662
Mdau akipata Ukodak na Models.
DSC_0683
Mama wa Mitindo nchini Asia Idarous Khamsin akipata ukodak na mwanamitindo Mustafa Hassanali kwenye After Party ya kuwashukuru wadau walioshiriki kwenye onesho la Lady in Red lililotimiza miaka 10 hivi karibuni.

waliotembelea blog