
12:50 AM

Unknown

12:13 AM

Unknown
EGYPT
wametinga Fainali ya AFCON 2017, Kombe la Mataifa ya Afrika, nah ii ni
mara yao ya 9 kufanya hilo na kuikuta Rekodi ya kucheza Fainali nyingi
baada ya Jana huko
Stade de I'Amitie, Libreville Nchini Gabon
kuibwaga Burkina Faso 4-3 kwa Mikwaju ya Penati Tano Tano kufuatia Sare
ya 1-1 katika Dakika 120.
Kipa Vterani wa Egypt, Essam El Hadary,
mwenye Miaka 44, ndie alikuwa Shujaa kwa kuokoa Penati ya Bertrand
Traore na kuwapa Egypt ushindi.
Katika
Mechi hiyo, Egypt walitangulia kufunga kwa Bao la Dakika ya 65 la
Mohamed Salah na Burkina Faso kusawazisha Dakika ya 72 kupitia Aristide
Bance.
Kwenye Fainali, Egypt watapambana na Mshindi kati ya Ghana na Cameroon wanaopambana Leo huko Libreville, Gabon.
VIKOSI:
BURKINA FASO:Koffi,
Yago, Dayo, B. Koné, Y. Coulibaly, Kaboré, I. Touré, R. Traoré (Diawara
80'), B. Traoré, Bancé (A.Traore 102'), Nakoulma.
EGYPT:El-Hadary,
El Mohamady (Gaber 106'), Hegazy, Gabr, Fathy, Hamed, M. Salah, I.
Salah, Said, Trezeguet (Sobhi 85'), Kahraba (Warda 76')
AFCON 2017
RATIBA
Robo Fainali
Jumamosi Januari 28
Burkina Faso 2 Tunisia 0 [RF 1]
Senegal 0 Cameroon 0 [Penati 4-5] [RF 2]
Jumapili Januari 29
Congo DR 1 Ghana 2 [RF 3]
Egypt 1 Morocco 0 [RF 4]
Nusu Fainali
Jumatano Februari 1
Burkina Faso 1 Egypt 1
Alhamisi Februari 2
2200 Cameroon v Ghana
Mshindi wa 3
Jumamosi Februari 4
2200 Burkina Faso v Aliefungwa NF 2
Fainali
Jumapili Februari 5
2200 Egypt v Mshindi NF 2
NCHI ZILIZOWAHI KUTWAA UBINGWA WA AFRIKA:
-Egypt-Mara 7
-Cameroon, Ghana-Mara 4
-Nigeria-Mara 3
-Congo DR-Mara 2
-Zambia, Algeria, Congo, Ethiopia, Ivory Coast, Morocco, South Africa, Sudan, Tunisia-Mara 1

12:12 AM

Unknown

12:11 AM

Unknown
Ligi
Kuu England imeendelea Jana kwa Mechi 3 na Manchester City kuibuka
washindi wakubwa kwa kuicharaza West Ham 4-0 wakati Manchester United
ikitoka 0-0 na Hull City na Stoke City na Everton kutoka 1-1.
Huko
London Stadium Jijini London, Wenyeji West Ham walibandikwa Bao 4-0 na
Man City kwa Bao za Kevin De Bruyne, David Silva, Gabriel Jesus na Yaya
Toure.
Matokeo hayo yamewabakisha City Nafasi ya 5.
Huko Old
Trafford, Kipa wa Hull City Eldin Jakupovic aliikosesha ushindi Man
United kwa kuokoa Bao za wazi kadhaa na hasa michomo ya Zlatan
Ibrahimovic na Paul Pogba.
Matokeo
hayo yamewabakisha Man United Nafasi ya 5 ingawa hawajafungwa katika
Mechi zao 14 zilizopita za Ligi lakini Sare hii ya 3 mfululizo ndio
inawatafuna na kuwabakisha Nafasi hiyo ya 6 wakiwa Pointi 4 nyuma ya
Timu ya 5 City na Liverpool zinazofungana kwa Pointi.
Huko
Britannia Stadium, Wenyeji Stoke City na Everton zilitoka Sare 1-1 na
Wafungaji walikuwa Peter Crouch kwa Stoke na Ryan Shawcross aliejifunga
mwenyewe kuisawazishia Everton.
Kwa Crouch, hilo lilikuwa Bao lake la 100 la Ligi.
EPL – Ligi Kuu England
RATIBA
Jumamosi Februari 4
1530 Chelsea v Arsenal
1800 Crystal Palace v Sunderland
1800 Everton v Bournemouth
1800 Hull City v Liverpool
1800 Southampton v West Ham United
1800 Watford v Burnley
1800 West Bromwich Albion v Stoke City
2030 Tottenham Hotspur v Middlesbrough
Jumapili Februari 5
1630 Manchester City v Swansea City
1900 Leicester City v Manchester United

12:10 AM

Unknown
Emmanuel Adebayor amejiunga na Timu ya Istanbul Basaksehir