Tuesday, April 7, 2015
1:13 AM
Unknown
Maandamano ya Wanamichezo wa timu mbili za Wakaguzin na Wadhibiti wa hesabu za Serekali wa Zanzibar na Tanzania wakipita kwa maandamano wakati wa ufunguzi wa michezo yao iliofanyika uwanja wa amaan Zanzibar timu ya CAG Tanzania imeshinda mchezo wa mpira kwa mabao 7--0.
Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serekali Tanzania Profesa Mussa Juma Asad akiwa na Maofisa wa CAG wakati akiendea kuzindua rasmin michezo hiyo iliofanyika uwanja wa Amaan Zanzibar
Maofisa wa CAG Zanzibar na Tanzania wakiwaenda uwanjani kwa ajili ya uzinduzi wa michezo hiyo
1:11 AM
Unknown
Kikundi mahiri cha KAPOTIVE Star Singers kutoka Mjini Bukoba leo kimefanya Tamasha kubwa la Pasaka kwenye Mji wa Geita katika Ukumbi wa GEDECO na kushuhudiwa na Umati wa Watu wengi zikiwemo Kwaya mbalimbali za hapa Geita na Waumini mbalimbali na kuifurahia Pasaka hiyo ambayo ni Alama ya Ukombozi wa Mwanadamu dhidi ya Dhambi kupitia kifo na Ufufuko wa Yesu Kristo. Wana'KAPOTIVE walisindikizwa na kwaya ya Mt. Thomas wa Aquino na Aaron Entertainment wa hapo Geita. Watu walivutiwa sana na kiwango cha juu ya kikundi cha KAPOTIVE mpaka wengine wakadiriki kusema sio kutoka Bukoba.
Watu hawakuweza kujizuia na kuanza kujimwaga kwa muziki wa Yesu, palikuwa hapatoshi!!!!
Vijana
machachari wa Kapotive Star Singers, Denis Deus na Claudius Mutabuzi
wakilikamatilia jukwaa kwa mbwembwe zote ilimradi kuwakamata watazamaji
waliofurika ukumbi wa GEDECO.
Mambo si ndo hayo!!!!
1:08 AM
Unknown
Kundi zima la Yamoto Band punde walitinga Katika Kituo cha Radio Kasibante 88.5 Bukoba kuongea moja kwa moja na Wakaazi wa Bukoba juu ya Shoo ya yao inayotarajiwa kufanyika Usiku huu katika Ukumbi wa Burudani wa Lina's Night Bukoba. Bendi inayokuja kasi hapa Nchini inayoundwa na Vijana Machachari kama Aslay, Becka, Bella na Maromboso wameteta na Wanabukoba kwamba waje kwa wingi katika Ukumbi huo wa Lina's wajionee walichokuja nacho kipya katika Pasaka hii ya pili maana kwa sasa watawasha Moto wa Uhakika na Watatoa Burudani Live jukwaani na wamekuja wamejipanga wakiwa na Vijana wengine ambao ni Maalum kwa Kuliteka Jukwaa kwa mapigo ya Live"
Mtandao huu wa jamii murua kwa habari tamu za Michezo na Burudani pia umeweza kuzinyaka za haraka haraka kwamba baada ya Shoo ya leo katika Ukumbi wa Lina's Kesho Jumatatu watatoa Burudani pia huko Biharamulo kwa kiingilio cha 10,000/ siku ambayo ni Karume Day" ya jumanne tarehe 07/04/2015. Kiingilio cha Shoo ya leo ya Lina's kwa kawaida ni Tsh 10,000/ na VIP ni Tsh.15,000/-
Subscribe to:
Comments (Atom)
RSS Feed
Twitter