Xabi Alonso, Kiungo wa Real Madrid, ametangaza kustaafu kuichezea Nchi yake Spain.Alonso, Miaka 32, amekuwa mmoja wa kiini cha mafaniko ya Spain iliyotwaa EURO 2008 na EURO 2012 pamoja na Kombe la Dunia huko Afrika Kusini Mwaka 2010.
Juzi Alonso aliichezea Spain Mechi yake ya 112 ilipofungwa 2-0 na Chile kwenye Mechi Kundi B na kutupwa nje ya Fainali za Kombe la Dunia huko Brazil.

Kwenye Mechi hiyo, Alonso alibadilishwa wakati wa Mapumziko baada kupwaya na kupokonywa Mpira uliozaa Bao la Kwanza la Chile.
Lakini Alonso ndie Mchezaji pekee aliewafungia Spain Bao pekee kwenye Mashindano haya huko Brazil alipofunga kwa Penati kwenye Mechi ya Kwanza ya Kundi B waliponyukwa Bao 5-1 na Netherlands.

Mara baada ya Spain kutupwa nje ya Fainali ya Kombe la Dunia, Alonso alisema: “Vitu vinabadilika. Zama zinaisha kwa kufungwa…na hiki kilikuwa kipigo kichungu. Hatukutegemea lakini ndio mchezo. Hivi vitu vinatokea. Hatukutegemea lakini ni lazima tuyakabili majonzi yetu vile vile kama tunavyofurahia, kama Wanaume.”
Aliongeza: “Tumecheza dhidi ya Timu zilizojitayarisha vyema na sasa tunarudi nyumbani. Inauma lakini huu ndio mpira. Kama nilivyosema, tulijua namna ya kushinda, sasa inabidi tujue namna ya kushindwa!”
Mbali ya Alonso kutangaza kustaafu pia kuna wasiwasi kuwa Kiungo Xavi na Kipa Iker Casillas, ambao wote wamecheza ovyo huko Brazil, wanaweza kufuata nyayo zake.
Zipo habari kuwa Kocha wa Spain, Vicente del Bosque, hasa kwa vile Shirikisho la Soccer la Spain, RFEF, linaunga mkono aendelee na kazi yake.
KUHUSU REKODI YA XABI ALONSO
BORN: Tolosa, Spain, November 25, 1981
1999-2000: Real Sociedad B (39 apps, 2 gls)
1999-2004: Real Sociedad (114 apps, 9 gls)
2000-2001: Eibar (loan) (14 apps, 0 gls)
2004-2009: Liverpool (143 apps, 15 gls)
2009-NOW: Real Madrid (158 apps, 4 gls)
2003-NOW: Spain (112 caps, 16 gls)
CLUB HONOURS:
LIVERPOOL - FA Cup (2006), FA Community Shield (2006), Champions League (2005), UEFA Super Cup (2005)
REAL MADRID - La Liga (2012), Copa del Rey (2011, 2014), Supercopa de Espana (2012), Champions League (2014)
SPAIN - World Cup (2010), European Championship (2008, 2012)
RSS Feed
Twitter
2:59 AM
Unknown
1-0,
Peter Odemwingie kushoto akishangilia bao lake lililotosha kuwapatia
alama 3 muhimu na kuwawezesha kuwa na jumala ya pointi 4 na wako nafasi
ya pili kwenye kundi lao na mtanange ujao kwa Nigeria ni jumatano tarehe
25 saa moja kamili.
Warembo
wanaowania taji la mkoa wa Tanga, Nice & Lovely Miss Tanga 2014
wakijiaandaa kufanya usafi katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga, ikiwa
ni moja ya kampeni ya kuendelea kulifanya jiji hilo liwe safi muda wote.
Washiriki
wa Nice & Lovely Miss Tanga 2014 wakitupa takataka katika gari
maalum la kubeba taka. Mshindi wa kwanza katika shindano hilo atapata
zawadi ya gari dogo aina ya Toyota Vitz.
Zoezi
la usafi limepamba moto na kuliacha eneo hilo safi kabisa. Mgeni rasmi
katika shindano hilo atakuwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mheshimiwa Chiki
Gallawa. 
Suarez baada ya kuimaliza England kwa bao 2-1.
Patashika..Kipindi cha kwanza

Meneja wa England Hodgson


Ligi kuu England itaanza Agosti 16 na leo hii Ratiba ya Msimu mpya wa 2014/15 imetangazwa.
Man United na Meneja wao mpya kutoka Holland, Louis van Gaal kuiongoza Manchester United wakiwa Nyumbani Old Trafford. 


Zawadi yeu hii...1-0!!Aguero na mwenzake wakishangilia bao mapeeema huku wachezaji wa Bosnia-Herzegovina (kushoto) wakijiuliza!
Lionel Messi akipongezwa baada ya kupiga frii kiki iliyosababisha mpaka Kolasinac kujifunga bao langoni mwao.
Mashabiki wa timu ya Argentina wakiipa sapoti timu yao usiku huu!! 

Rais Kenyatta akiongea na Wachezaji wa Timu hiyo.
Hapa Akigawa tiketi huku akishuhudiwa na mkewe Bi. Margaret Kenyatta na seneta wa Nairobi Mike Sonko (kushoto).
Picha ya Pamoja.



Darly Janmaat na Diego Costa wakiendana sambamba
Wasley Sneijder akifanya yake
Sergio akiwekewa kigingi na Nigel
Diego Costa vipi...unasababisha penati...
Mzee Mzima Alonso ndie aliyeipa bao kwa mkwaju wa penati Spain
Xabi Alonso akishangilia bao
Van Persie akitupia kusawazisha...1-1
1-1....Van Persie akimpagawisha kipa wa Spain kwa bao la kiwango
Van Persie akishangilia bao lake
Nipe tano bosi wangu!! Nilikwambia!! leo ni chinja chinja!!
Robben akitupia..
Kipa Cassilas leo hii kama mtoto !!
Mpaka ndani ya nyavu!! bao la tatu
Stefan akipeta baada ya kufunga bao
Van Persie tena...
Chupuchupu!!
5-1