TIMU ya Coastal Union imewasili
jijini Tanga ikiwa na mikakati mizito ya kuhakikisha inawanyamazisha
wapinzani wao Azam FC ikiwa ni muendelezo wa Michuano ya Ligi kuu soka
Tanzania bara mchezo unaotarajiwa kucheza kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani
wikiendi ijayo.
Akizungumza leo na waandishi wa
habari, Ofisa Habari wa Coastal Union,Oscar Assenga amesema kuwa sasa
nguvu zao watazielekeza kwenye mchezo huo utakaochezwa kwenye mjini
hapa.
Amesema kuwa dhamira yake
aliyoipanga ni kuchukua pointi tatu muhimu dhidi ya Ruvu Shooting
haikuweza kutimia na kujikuta wakilazimishwa sare ya kufungana bao 1-1
hivyo atahakikisha inatimia kwenye mechi hiyo.
Amesema timu hiyo imerudi salama
mkoani hapa na tayari wameshaanza kujipanga imara kuhakikisha mechi hiyo
timu inapata ushindi n kutokana na uimara wa kikosi chao
Aidha amesema kuwa wachezaji wa
kikosi hicho wameimarika zaidi na wapo imara kuweza kupambana kufa na
kupona ili kuchukua pointi tatu muhimuzo zitawasogeza kwenye nafasi za
juu kwenye msimamo wa Ligi hiyo.
Hata hiyo amewataka wapenzi na
mashabiki wa soka mkoani hapa kuhakikisha wanajitokeza kwa wingi katika
mchezo huo ili kuipa hamasa timu hiyo kuweza kutimiza ndoto zake.
Mwisho.
RSS Feed
Twitter
3:19 AM
Unknown

Rooney akishangilia kwa Mashabiki Old Trafford baada ya kuifungia bao la tatu Man United mbele ya Mashabiki 75,112.
Boxing!!
Rooney akishangilia kwa aina yake baada ya kuifungia bao la mwisho Man United leo dhidi ya Spurs
Dakika
ya 34 Kepteni Wayne Rooney alipiga Bao la 3 alipounasa Mpira karibu ya
Mstari wa Kati na kuwapita Mabeki wa Spurs Dier na Rose na kisha
kumhadaa Kipa Hugo Lloris na kufunga.
Mara
baada Mpira kutinga wavuni, Rooney alishangilia kwa kucheza Ngumi na
kisha kujidondosha chini akivunga amepigwa Ngumi na kuzirai ikiwa ni
jibu la habari zilizozagaa mitandaoni hii Leo kuwa alipigwa Ngumi na
kuzirai Jikoni Nyumbani kwake wakati akifanya mzaha wa kucheza Ngumi na
Mchezaji wa zamani wa Man United Phil Bardsley ambae sasa anacheza Stoke
City.
Rooney chini akipongezwa na Ashley Young
3-0

Juan Mata akichuana
Marouane Fellaini akipongezwa na Mata
United wakiendesha! Michael Carrick akiwaongoza baada ya kufunga bao la pili kushangilia.
2-0

Fellaini akishangilia baada ya kufunga bao la kwanza

Harry Kane hakuonekana leo..kafunikwa Old Trafford
Baadhi ya Wachezaji wa Chelsea akiwemo Terry wakiwa vichwa chini baada ya kugawana pointi na Sant's
Mpaka dakika zinayoyoma ilikuwa ni 1-1
John Terry akiwa hoi!!
1-1
Dusan Tadic hakufanya makosa!
John Terry hapa alikosa bao wazi..
Hapa ni England Diego Costa!!
Chelsea Chupuchupu wapate bao hapa...mpira uligonga nguzo
Kashikashi
ilitokea ndani ya eneo hatari la penati na Southampton mchezaji wake
kuangusha na hatimae kupata penati na kusawazisha kwa mkwaju huo wa
penati kupitia kwa Dusan Tadic.
Kipindi cha kwanza dakika 11 Diego Costa aliipatia bao kwa kichwa Chelsea na kufanya 1-0 dhidi ya Southampton.