
HOFU kubwa imetawala Kanisa Katoliki Parokia ya Uru iliyopo Wilaya ya Moshi Vijijini mkoani Kilimanjaro, kutokana na matukio kadhaa yanayoendelea kutokea katika kanisa hilo huku baadhi ya watu wakiyahusisha na imani za kishirikina.
Katekista wa parokia hiyo, Lucian Tesha, aliwaambia waamini waliokusanyika katika ibada ya misa ya kwanza kanisani hapo juzi Jumapili kuwa usalama katika kanisa hilo upo shakani na kuwataka kuwa macho.
Hali hiyo inatokana na kile alichodai kuwa kuna mtu mmoja (mwanaume) kwamba amekuwa akionekana eneo la kanisa akiweka vitu mbalimbali ambavyo havina nia njema na kanisa hilo la Moyo Mtakatifu wa Yesu.
“Mtu huyu ameonekana kanisani hapa kwa mara ya nne sasa, hatujui anataka nini, lakini amekuwa akiweka vitu mbalimbali katika sanamu ya Bikira Maria na karibu na sakristi ya mapadri…kwa kweli hali hii inatisha.
"Ninawaomba tunapotoka kanisani hapa tuende kuangalia katika sanamu hiyo, kwani mtajionea vitu hivyo na wakati mwingine hata kadi za pikipiki,” alisema Tesha na kuacha waamini wakinong’ona.
Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana kanisani hapo ni kuwa tangu paroko mpya aingie katika parokia hiyo, aliyefahamika kwa jina moja la Kiondo kumekuwa na matukio ambayo si mazuri.
“Tangu aingie hapa sanamu ya Mtoto Yesu imeibiwa na watu wasiofahamika… hatujakaa vizuri yanajitokeza haya mauzauza ya watu kuweka vitu visivyofahamika kanisani.
“Haifahamiki kama wanampima au la, lakini wengi wanajiuliza ni kwa nini matukio haya hayakuwapo siku zote? Alihoji muumini mmoja.
Siku za hivi karibuni kumekuwa na matukio ya makanisa kushambuliwa na hivyo kuwaweka roho juu waamini na mapadri wanapokuwa wakishiriki ibada takatifu
RSS Feed
Twitter
6:11 AM
Unknown
United wakishangilia

Mashabiki huko Hong Kong wakiipamba Manchester United baada ya kufunga bao 3-0 kabla ya mapunziko.
United wakishangiliwa baada ya kuifunga timu ya Kitchee bao la pili
Lam Ka Wai wa Hong Kong akipongezwa dakika ya 53 baada ya kuipatia timu yake bao na kufanya 3-1 kipindi cha pili.
Mchezaji wa Kitchee Huang Yang akishindwa kumkaba Anderson wa Man United hapa
Smalling akipiga mpira kwa kichwa hapa
Uwanja ulijaa matope na hapa Smalling kwenye patashika akizuia mchezaji wa Kitchee asipite na mpira
Uwanja unavyooneka hapa kimatope matope zaidi!!
Evra nae hakusita kuonesha mambo yake hapa mbele ya mchezaji wa Kitchee Tsang Kam Ko
Smalling akizungukwa hapa!
David Moyes kulia akiwa kwenye benchi pamoja na viongozi wasaidizi
Fabio Da Silva akikimbiza hapa!!
Tsang Kam hoi kwa Wilfried Zaha hapa!!
Mapema mashabiki wa United walionekana kwa furaha hapa na walionesha furaha ya kushinda tangu mapema














William O. Rutta (kulia) akiwa na Shabiki wa Taifa Stars
Chinja shingo!! 


























