
2:42 AM

Unknown
Kitendo cha Chadema kutetea viti vyake vinne vya udiwani kwenye uchaguzi
mdogo wa juzi, kimetafsiriwa kwamba ni kumfanya Meya wa Jiji la Arusha,
Gaudence Lyimo kukalia kuti kavu..bofya hapa kupata habari kamili

12:03 AM

Unknown
Maelfu
ya watu walifika hospitali binafsi ya uzazi kwenye jiji la Kotaworo eneo
la Bida, iliyopo jimbo la Niger jana Jumapili, kwa lengo la kwenda
kumshuhudia mtoto wa kike aliyezaliwa akiwa amevaa rozari ya Kiislamu
(Tasbihi) shingoni mwake.
Inaelezwa
kwamba mama wa mtoto huyo ambaye ana miaka ya kati, Adijat, alikimbizwa
hospitali karibu na nyumbani kwa Pa Mohammed Bello Masaba, mda wa saa 8
mchana na baada ya pilika za uzazi alifanikiwa kujifungua mtoto huyo.
Kwa
mujibu wa mmiliki wa hospitali hiyo ya uzazi, Alhaji Abubakar Baiwa
Shasha ambaye ndiye aliyesimamia zoezi hilo la kujifungua alisema,
“Nilishtuka nilipona mtoto anatoka akiwa na Tasbihi shingoni mwake, na
wakati wa uzazi mtoto alizaliwa akiwa na Rozari nyeusi.” Alisema Shasha.
“Ila nilishangaa baada ya muda rozari hiyo ilibadilika na kuwa nyeupe huku kukiwa na watu wengine wamezunguka.”
“Mara
baada ya habari hiyo kusambaa mjini, maelfu ya watu walifika kwenye
hospitali hiyo ya uzazi huku wakisema “Allahu Akibar; Allahu Akibar
(Mungu ni Mkubwa) huku wakifika na kumgusa mtoto huyo.”
Juhudi
za kumpata Baba wa mtoto huyo aitwaye Isah, ambaye anatokea eneo la Loma
ndani ya Jimbo la Kwara State wzilishindikana baada ya kukataa kuongea
na mtoa habari.
Mwanachuo
mmoja wa Kiislamu, Malam Idiris Ndajiwo alisema, kuzaliwa kwa mtoto
huyo akiwa na rozari “inaonyesha ukuu wa Allah. Kuzaliwa kwa mtoto huyu
leo, kwenye mji huu na eneo hili (Kutaworo) ni kitu kikubwa kwa
Waislamu. Hii hakika inakuja kuonyesha kwamba Allah ndiye mwenye kupanga
kwa lolote kutokea kwa yeyote kwenye ulimwengu huu.”