MABINGWA wa Italy Juventus wamesisitiza Kiungo wao Paul Pogba hauzwi licha ya Ofa kutoka Barcelona. Joan Laporta, Rais wa zamani wa Barca ambae sasa anagombea tena nafasi hiyo, ameweka kwenye ajenda yake kuwa akichaguliwa Urais basi atamnunua Pogba.
Laporta yupo kwenye kinyang'anyiro cha kugombea Urais pamoja na Rais wa sasa Josep Maria Bartomeu, August Benedito na Toni Freixa.
Pogba, Kijana wa Miaka 22 wa Kifaransa alietokea Man United kwenda Juve, pia anawindwa na Manchester City na Chelsea.
Mkurugenzi wa Juve, Giuseppe Marotta, amesema: "Yeyote anaemtaka Pogba anapaswa kuongea na sisi na si Wakala Mino Raiola. "
Aliongeza: "Tumezungumza na Barca katika Miezi ya hivi karibuni lakini hauzwi. " Hata hivyo, hata kama Barca watamnunua Pogba ambae ana Mkataba hadi 2019, hawawezi kumtumia hadi Januari 2016 kutokana na kufungiwa na FIFA kwa kukiuka Kanuni za Usajili wa Wachezaji Chipukizi.
Licha ya Adhabu hiyo, Barca imeshasaini Wachezaji Wawili katika Kipindi hiki cha Uhamisho ambao ni Aleix Vidal kutoka Sevilla na Kiungo wa Uturuki anaetokea Klabu ya Atletico Madrid Arda Turan.
RSS Feed
Twitter
11:38 PM
Unknown


Kipa mpya wa Arsenal Petr Cech
Arsene Wenger akiwaangalia Vijana wake kwenye mazoezi
Mtu kati!
Cazorla wakati wa mapumziko
Raheem
sterling kwa furaha akiteta jambo na Wenzake alipofanya Mazoezi kwa
mara ya kwanza tangu ajiunge na Klabu hiyo ya Manchester City huko
Australia kwenye Ziara.
Wachezaji wa City wakifanya mazoezi kujiandaa na Msimu mpya wa 2-15/2016
Kwa Mara ya Kwanza
Yaya Toure nae alikuwemo kwenye mazoezi
Sterling katikati akifanya zoezi
Ni mazoezi kujiandaa na mechi za kirafiki katika kujiandaa na msimu mpya ujao
Mazoezi ya nguvu









Naibu
Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Msafiri Mtemelwa (kushoto) akimkabidhi
kadi msanii maarufu wa filamu nchini, Mohamed Mwikongi jina la sanaa
'Frank' alipotambulishwa mara baada ya kujiunga na chama hicho.
Naibu
Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Msafiri Mtemelwa (kushoto) akimkabidhi
aliyekuwa Mwenyekiti wa kitengo cha vijana Taifa wa NCCR Mageuzi, Deo
Meck alipotangazwa kujiunga na chama hicho rasmi leo jijini Dar es
Salaam.
Naibu
Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Msafiri Mtemelwa (kushoto) akimkabidhi
kadi na katiba msanii maarufu wa filamu nchini, Mohamed Mwikongi jina la
sanaa 'Frank' alipotambulishwa mara baada ya kujiunga na chama hicho.
Naibu
Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Msafiri Mtemelwa akizungumza na waandishi
wa habari leo alipowapokea baadhi ya wanachama wapya wa ACT-Wazalendo.
Kushoto ni Katibu wa Kampeni na Uchaguzi, Mohamed Masaga na kulia ni Deo
Meck mwanachama mpya wa ACT Wazalendo.
Diego Costa ndani ya Uzi mpya
Kumeibuka
ripoti ya Liverpool kuja juu kuipiku Manchester United kwa kukubali
kutoa Pauni Milioni 32.5 kumnunua Straika wa Aston Villa Christian
Benteke.
Tayari
Liverpool imeshanunua Wachezaji wengine 6 kwa ajili ya Msimu ujao ambao
ni Nathaniel Clyne, Roberto Firmino, Danny Ings, Adam Bogdan, Joe Gomez
na James Milner.