Pichani kati msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka THT, Rachael akiwa
na madansa wake wakilishambulia jukwaa kwa namna ya kipekee usiku huu
kwenye tamasha la Fiesta ndani ya uwanja mdogo wa Kambarage mjini
Shinyanga.
Mmoja wa wasanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya,atambulikae kwa jina
la kisanii Ommy Dimpo akiwaimbisha mashabiki huku akisherehekea siku
yake ya kuzaliwa na wakazi wa mji huo usiku katika tamasha la Fiesta
ndani ya uwanja mdogo wa Kambarage
Mmoja wa wasanii wa Bongofleva anaefanya vyema katika muziki huo
atambulikae kwa jina la Young Killer a.k.a Msodoki akiimba jukwaani
usiku huu kwenye tamasha la Fiesta ndani ya uwanja mdogo wa Kambarage
mjini Shinyanga.
Pichani juu na chini ni umati wa wakazi wa mji wa Shinyanga
waliojitokeza kwa wingi kwenye tamasha la Fiesta ndani ya uwanja mdogo
wa Kambarage,usiku huu.
Wasanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya,Ney Wa Mitego (pichani kulia)
na Stamina wakilishambulia jukwaa kwa wimbo wao wa Huko Kwenu vipi,huku
makele ya shangwe yakiwa yametawala kila kona ya uwanja mdogo wa
Kambarage mjini Shinyanga usiku huu.
Sehemu ya mashabiki wa Fiesta wakishangilia yaliyokuwa yakijiri kwenye
jukwaa la Fiesta 2014 ndani ya uwanja mdogo wa Kambarage mjini
Shinyanga.
Mwanadada Linah akionesha umahiri wake wa kucheza wimbo wake wa Ole
Temba juu ya jukwaa la Fiesta 2014 usiku huu kwenye tamasha la Fiesta
ndani ya uwanja mdogo wa Kambarage.
Ukipenda muite Mr Blue,msanii wa muziki wa kizazi kipya juu ya jukwaa
la Fiesta 2014 usiku huu ndani ya uwanja mdogo wa Kambarage mjini
Shinyanga.
Mmoja wa wasanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya,atambulikae kwa jina
la kisanii Ommy Dimpo akiimba mbele ya mashabiki wimbo wake wa ani kama
mama usiku huu katika tamasha la Fiesta ndani ya uwanja mdogo wa
Kambarage
Wanajiita Wakata Mkaa kutoka kundi la Wanaume TMK,Chege na Temba kwa
pamoja wakilishambulia jukwa la fiesta mbele ya umati wa watu (hawapo
pichani) ndani ya tamasha la Fiesta lililofanyika usiku huu ndani ya
uwanja mdodog wa Kambarage mjini Shinyanga.
Wasanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya Khadija anaetamba na wimbo
wake wa maumivu akiwa sambamba na mwanadada Rachael anaetamba na wimbo
wake wa Ole temba,kwa pamoja wakilishambulia jukwaa la Fiesta usiku huu
ndani ya uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.
Mmoja wa wasanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya,atambulikae kwa jina
la kisanii Ommy Dimpo akiwaimbisha mashabiki wimbo wake wa nani kama
mamaa,usiku huu kwenye tamasha la Fiesta ndani ya uwanja mdogo wa
Kambarage
Sehemu ya umati wa watu wakishangweka na na Fiesta usiku huu.
Mmoja wa wakali wa kukamua mangona kutoka Clouds FM,Dj Zero akikamua
ngoma jukwaani mbele ya umati wa wakazi wa Shinyanga kwenye tamasha la
Fiesta ndani ya uwanja mdogo wa Kambarage
Sehemu ya umati wa wakazi wa mji wa Shinyanga wakiwa ndani ya uwanja
mdogo wa Kambarage,wakishuhudia tamasha la Fiesta 2014 likifanyika usiku
huu.
Sehemu ya umati wa wakazi wa mji wa Shinyanga wakiwa ndani ya uwanja
mdogo wa Kambarage,wakishuhudia tamasha la Fiesta 2014 likifanyika usiku
huu.