
Meneja wa kilabu ya Manchester United Louis Van Gaal anaamini kwamba timu yake itatumia fursa ya kushuka kwa soka ya kilabu ya Manchester City katika uwanja wa Etihad kuishinda kilabu hiyo.
Kilabu ya Manchester City imepoteza mechi zake mbili za mwisho baada ya kushindwa na West Ham na Newcastle.
''Kile tulichokiona katika mechi mbili za mwisho si matokeo ya kuridhisha,alisema Van Gaal.
''Tuna hisia njema kuhusu mechi hii''.''Tunahitaji matokeo mazuri na huenda yakawa dhidi ya Manchester City''.Aliongezea Van Gaal.

City iko katika nafasi ya tatu wakiwa nyuma kwa alama sita dhidi ya Chelsea.
Tangu ipoteze kwa mabao 5-3 dhidi ya Leicester mnamo Septemba 21,Manchester United haijapoteza na huenda ikaikaribia Mancity katika nafasi ya nne iwapo itashinda mchuano huu wa 'Derby'.
Hatahivyo ushindi dhidi ya Manchester United utakuwa wa nne kati ya timu hizo mbili hatua ambayo haijaafikiwa kwa takriban miaka 44 na timu hiyo.
RSS Feed
Twitter
8:11 AM
Unknown
Wachezaji wa Man City wakishangilia na kupongezana kwa bao lililofungwa na Aguero dakika 63
Smalling ameoneshwa kadi nyekundu kipindi cha kwanza mwishoni dakika 39
Ni Shida kwenye lango la Man United.
Kipa wa United De Gea bado ni shida...kwenye hii Debi!!
Wayne Rooney arudi kwenye Debi ya Manchester United

