Ligi Kuu Vodacom, VPL, Leo ipo dimbani kwa Mechi 3 za Jijini Dar es Salaam, Mbeya na huko Tanga huku Yanga wakiwa na nafasi poa kutwaa uongozi wakishinda.
Yanga Leo watakuwa Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam kucheza na Kagera Sugar na ushindi kwao utawashusha Mabingwa Watetezi Azam FC kutoka kileleni.

Lakini Kagera Sugar ni Timu ngumu ambayo katika Mechi ya kwanza ya Ligi Msimu huu iliichapa Yanga 1-0 huko Kaitaba, Bukoba.
Simba Leo hii wako huko Mkwakwani Tanga kuivaa Mgambo JKT wakiwa kwenye wimbi la ushindi wa Mechi 3 mfululizo kwa kuzichapa Tanzania Prisons 5-0, Yanga 1-0 na Mtibwa Sugar 1-0 ambalo limewafanya wajikite Nafasi ya 3.
Huko Sokoine, Mbeya, wana wa Nyumbani Mbeya City wataivaa Timu isiyotabirika Stand United ya Shinyanga.
VPL inaongozwa na Azam FC wenye Pointi 33 kwa Mechi 17 wakifuata Yanga wenye Pointi 31 kwa Mechi 16 na Simba ni wa 3 wakiwa na Pointi 29 kwa Mechi 18.
RATIBA YA MECHI ZA LEO:
Jumatano Machi 18
Yanga v Kagera Sugar
Mgambo JKT v Simba
Mbeya City v Stand United
RSS Feed
Twitter
6:04 AM
Unknown
Manchester City wana kibarua kigumu kusonga Robo Fainali ya UEFA CHAMPIONS LIGI kwa mara yao ya kwanza kabisa.
Kwenye
Mechi hiyo ambayo Barca walitawala, City wangekuwa na kazi ngumu zaidi
kama si uhodari w Kipa wao Joe Hart kuokoa Penati ya Dakika za Majeruhi
ya Lionel Messi.
Kwa
City hali hivi sasa ni tete na Jumamosi walipigwa 1-0 na Timu ya mkiani
Burnley na kuharibu matumaini yao ya kutetea Taji lao la Ubingwa wa
England. 
Kwenye
Mechi hii Barca itamkosa Majeruhi Sergio Busquets na hivyo Jeremy
Mathieu kucheza badala yake na hili litamfanya Javier Mascherano acheze
kama Kiungo Mkabaji.
City itamkosa Fulbeki wake Gael Clichy ambae yupo Kifungoni baada ya kutolewa kwa Kadi Nyekundu katika Mechi ya kwanza.
Nje!
Kocha Wenger akitoka Uwanjani baada ya kupokea matokeo
Gibbs akiwa kichwa chini!
Mdebwedooo!
Masikitiko Makubwa!!
Kilio kwa Mesut Ozil!!
Upande mwingine furaha ....harusi!!
Kocha wa As Monaco akiwa aamini!!
Mtajiju!! Tunasonga mbele sisi!!

Yannick Ferreira Carrasco akishangilia baada ya mpira kumalizika 

Giroud aliwapa matumaini baada ya kufunga bao lakini mambo yakawa tofauti kwenye bao la Ugenini